SHINA LA UKOO NA URITHI.
Imeandaliwa na mr.luhwago shadrack c mwanafunzi wa
sayansi ya chakula na teknolojia SUA (2013-2016)
Mawasiliano: 0764444277, luhwagoshadrack17@gmail.com
UTANGULIZI.
Somo hili ni pana na lina mafundisho jinsi ya kutambua
jinsi dhambi mbali mbali zinavyoweza kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine
,
Bila ya kizazi chenyewe
kutambua
MAANA
YA SHINA LA UKOO URITHI
Katika kichwa hiki cha somo tunatakiwa tujue maana ya
maswali yafuatayo
ü a/ nini maana ya shina
ü b/nini maana ya shina la ukoo
ü c/nini maana ya urithi
ü d/nani anarithishwa
ü e/ sifa za mwenye
kurithishwa
Shina lina maana ya
chanzo,
beginnner,
a source,
anzilishi
B.URITHI
ni hali ya kupokea sifa,
tabia, umbo, namna, kutoka kwa wazazi wako au ndugu yako
its known as inheritance(utu
wa ndani) genotypic characters
thus its automatically
urithi huu huambatana na
Damu(watu wa Damu moja yaani ndugu)
katika maisha yetu kuna watu
wawili(mtu wa ndani ambaye yupo rohoni na mtu
wa nje ambaye yupo katika
ulimwengu wa mwili)
ndiyo maana utasikia mwili
wa marehemu fulani………..kwani yeye anakuwa yupo wapi……..?
MWANZO WAKO NI UPI NA UKOJE..?
Kila kitu na mwanzo wake,
kusema kweli ni vigumu sana kuelewa mwanzo wako wa maisha na wakati
mwingine unakata tamaa ya kutokuendelea
kufuatilia the orign of life.
Maisha yangu (luhwago
shadrack c) kusema kweli nilipata shida sana namna ya kuweza kupata habari na
taarifa yakinifu juu ya kuzaliwa kwangu, juu ya ukoo wangu , kwa nini sisi ni
akina luhwago, je neno luhwago lina maana gani?, nani mwanzilishi wa jina hilo?
Na alikuwa anamaanisha nini juu ya jina hilo? Unajua nini……. TAMANI KUJUA……….
Siku moja katika huduma
yangu ya kufundisha injili nilikutana na mtoto mmoja ambaye ni mgonjwa
tukamuombea lakini ilishindikana. nikamuuliza mama yake juu ya kuzaliwa kwa
mtoto wake akanambia kuwa kipindi
amezaliwa mtoto wake aliugua sana karibu kufa ndipo alipochukua hatua ya kwenda
kwa miungu na kumlaza kwenye ngozi ya kondoo iliyochunwa muda huohuo ndipo
akapona “ tujiulize je alipona ? …..hapana maana kukua kwake kuliandamana na
kuugua.
Pia kuna dada mwingine
katika ukuaji wake alishawahi kuugua kiasi cha kubadilika sura yake akapelekwa
kwa mganga wa kienyeji. Alipoolewa alipata uwezo wa kuzaa mtoto, cha kushangaza
mtoto Yule alikuwa hakui(mwaka mmoja bado alikuwa ana kilogram 4).kilichofanyika
ni kumpeleka kwa yule mganga wa kienyeji na wakatamka maneno yafuatayo na
nukuu(tuliyemleta kipindi kile sasa anamtoto tunaomba na huyu mtoto
apokelewe pia)…….baada ya hapo anaendelea kukua hadi muda huu ninavyoandika
makala hii…. Je huyu mtoto ataishije…..?
B. KIZAZI CHA TERA.
Labda
ili uelewe ngoja nikupitishe katika maandiko . tuangalie kizazi cha Tera
mwazo11:24. Na kuendelea………..
Mwanzo 11:24 Tera anazaliwa na anazaa (Abrahamu ,Nahori na Harani) na wengineo akiwemo sarai
Abraham
akamuoa sarai(akawa tasa)
Rahani akamzaa milka
Nahori akamwoa milka akamzaa bethuel na wengineo
Sarai akamruhusu Abraham kuzaa na hagari kijakazi
wake akazaliwa Ishmael Kipindi
hagari ni mjamzito wakagombana na bibi yake sarai
Bethuel akamzaa Rebeka na Labani
Kwa
imani sarai akapata ujauzito uzeeni akamzaa isaka
Isaka akamuoa Rebeka(akawa tasa)
Kwa
kuomba na kumlilia Mungu rebeka
akapata ujauzito akazaliwa Esau na Yakobo
Esau
akapoteza nafasi yake ya uzaliwa wa
kwanza, yakobo akabarikiwa.
Labani
akamzaa Lea na Rahel
Yakobo
akamuoa Lea na Rahel (rahel akawa tasa
na ni mrembo) na siyo Lea
Esau
akaoa mkaanani akaleta uchungu ndani
ya nafsi ya wazazi wake
(Mungu
aliweka agano na Abraham kwamba wasije wakaoa wakaanani)
Lea
akapewa uwezo wa kuzaa hata kama ana sura mbaya.(akamzaa Reuben, simeoni, lawi
na Yuda) kila aliyezaliwa isipokuwa Yuda , lea anasema ili Yakobo mumewe ampende (yaani kamsahau Mungu)
na Yuda ndipo aliposema nitamsifu Bwana
Rahel
anaruhusu Yakobo azae na kijakazi
wake Bilha ili apate uzao
Kwa kumlilia
Mungu Rahel akapata mimba akamzaa Yusufu.
Lea
naye anaruhusu kijakazi wake zilpa aanze kuzaa na mumewe yakobo
(wanashindana kuzaa sasa) , wivu, tamaa,
upendo unakosekana ndani ya hizi familia
Katika
hili reubeni akalala na kijakazi wa aliyewahi kuzaa na baba yake yakobo
(yakobo akamlaani)
akapoteza pia nafasi yake ya uzaliwa wa kwanza.
Yuda anazini na mkwewe tamari
akijua ni kahaba wa mitaani na anazaliwa zera na pelesi
(wanagombana tumboni)
Mkono
wa Mungu unakuwa mzito juu ya Eri na onani kwa maana wametenda maovu mbele
za Bwana
Labda
nikuache hapa kwa Yuda , sasa tuangalie mambo yaliyomo ndani ya kizazi hiki:
- Utasa
- kuzaa na mjakazi (wajakazi) , uzinzi,
- kukosekana kwa upendo
- wivu na tama
- Uchungu
- Hasira
- Laana
SABABU ZA KUATHIRIWA KWA
KIZAZI CHA TERA
Tera
alikuwa mganga wa kienyeji
(Joshua 24:2) 2 Yoshua akawaambia watu wote, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi,
Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu,
naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine.
3 Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka
ng'ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake,
nikampa Isaka.
4 Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau;
nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri.
5 Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga
nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi.
hivyo kizazi chote cha Tera kilichofuata kilipata
kuathiriawa na vitu vifuatavyo, Utasa , kuzaa na mjakazi (wajakazi),
kukosekana kwa
upendo(29:30-31), wivu na tamaa(30:1), uchungu(26:34-35) , hasira(27:41) , Laana(49:3-4) na uzizi.
Kwa wewe unayesoma makala hii hakuna dhambi yenye
madhara na machukizo makubwa kwa Bwana kama kuabudu miungu mingine. Tazama haya…….,
YEREMIA 17:5-6
5 Bwana asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona
yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa
na watu
AYUBU (3:1)
Ayubu anailaani siku ya kuzaliwa kwake kwa sababu ya
taabu aliposema “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule
iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!
ZABURI 16:4)
Mtu asipo okoka au anaye abudu miungu mingine ugumu wa
maisha utaongezeka au mabaya yataongzeka
MITHALI 4:18
Mungu ansema usikubali kurithi upumbavu( maovu) Mjinga
hurithi upumbavu
MAMBO YA WALAWI 18:13
inasema
usifunue umbu la mama yako
hili linawalenga wanaozini na dada zao au wale ambao hawajaoa na kufanya
uasherati katika umri wao wa ujana au wazee wanaozini na ndugu zao
EZEKIELI 16:44
Katika maisha unatakiwa kuvunja madhabahu za urithi zinazo risishwa
kupitia maziwa ya mama kama inavyozungumziwa katika hapa ….inavyosema tabia ya mama itarithiwa na mtoto wake
ZABURI 51:5
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama
yangu alinichukua mimba hatiani.
YEREMIA 6:16
16 Bwana asema hivi,
Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia
hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda
katika njia hiyo.
MAOMBOLEZO 5:7
7 Baba zetu walitenda dhambi
hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu
yao
Sasa utakuwa umeanza
kuelewa ninachozungumza, Mungu akupe macho ya rohoni sana ili uweze kuelewa
maada hii: kwa muda huu tafuta majibu ya masuali haya; familia yako ina
ugomvi?, ina magonjwa yanayosumbua? Au wewe mwenyewe unasumbuliwa gonjwa ambalo
huponi?, kichwa au tumbo lako linakusumbua?, kuna tatizo la kuolewa au kuoa
katika familia yako?, katika familia yako kuna shida katika elimu?, familia
yenu kuna roho ya uzizi?, wivu?, ukahaba?, uchoyo?, tama?, vifo?, uchungu ndani
ya nafsi yako?,ulishanenewa maneno ya laana?, mabaya?, ya kutokufanikiwa?, je
jina lako lina maana gani?, lilitoka wapi na nani alikutajia?,hali ya imani ikoje katika familia yako?,
wanamwabudu Mungu yupi?, wanapopata matatizo wanakwenda wapi?, chukua hatua, ya
kuokoka, kutafuta toba ya kweli lasivyo maisha yako yatakuwa ya tabu.(soma kumb
28. yote namna laana na Baraka juu ya maisha yako).
MAMBO YA KUFANYA KUEPUKA ROHO ZA URITHI.
kuepukana na laana zote hizo hapo juu ambazo hadi leo
hii zinaendelea na hasa katika familia na koo zetu ambazo tumezaliwa
ü Kwanza kabisa peleleza mambo ya zamani (Yeremia 6:16)
ü Nenda mbele za Mungu kwa Toba ( Matendo 3:17)
Kwa hiyo yafuatayo ni mambo unaweza kuyafanya ili
kujiokoa na urithi wa mambo yaliyo orodheshwa hapo juu.
kwanza kuokoka na kumkiri Yesu kristo kwamba Bwana na mwokozi wa maisha yako
kwanza kuokoka na kumkiri Yesu kristo kwamba Bwana na mwokozi wa maisha yako
q kufunga na
kuomba (I Nyakati 7:14)
q kutoa sadaka
Mաaռʐօ ʍʐʊʀɨ ʍtʊʍɨsɦɨ......
ReplyDeleteamina kaka
DeleteThis is very good job.We often don't look onto these things in detail but what you have explained makes a lot of Sense.May the Almighty God bless you to continue with this kind of Services in Future.
ReplyDeleteAmen Dr.
ReplyDeleteAmen Dr.
ReplyDeleteHakika Mungu ni mkuu sana. Azidi kukutia nguvu.
ReplyDelete