Waebrania 4:16
"Basi na tukikaribie KITI CHA NEEMA kwa ujasiri, ili
tupewe REHEMA, NA KUPATA NEEMA YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI"
Ni habari njema mno kujua kuwa mbinguni hakuna kiti cha
hukumu tu.
Hakuna kiti cha enzi tu.
Pia kuna kiti cha neema. Kiti maalum ambacho kinaachilia
neema kwa walio ndani ya Yesu.
Ukimwendea Yesu
kama Mungu wa neema zote, huwa anaketi
kwenye kiti hiki na kuachilia neema kwa anayeihitaji.
Ni habari njema iliyoje kujua kuwa Mungu anapenda UPOKEE
NEEMA na ndiyo maana ana kiti maalum kwa ajili ya hilo; KITI CHA NEEMA.
Kama ambavyo benki kuna madirisha mbalimbali, yote yako
benki lakini yana kazi tofauti au kama vile hospitali kulivyo na madirisha
mengi na yana kazi tofauti, Vivyo hivyo Mungu anacho kiti maalum kwa ajili ya
NEEMA.
Hii itakuonesha ni kwa kiasi gani neema ni muhimu mno ili
mtu afanikiwe na afike kule Mungu amemuitia.
Angalia, hatusomi kokote kuwa mbinguni kuna KITI CHA MIUJIZA
AU KITI CHA UPONYAJI AMA KITI CHA IMANI, lakini kutokana na umuhimu wa neema,
Mungu ana KITI CHA NEEMA.
Na aina mojawapo ya neema anazotoa ni NEEMA YA KUTUSAIDIA
WAKATI WA MAHITAJI.
Neema maalum ambayo tunaipokea kabla mahitaji hayajaja, na
yakija yanatukuta tuko WELL EQUIPED AND EMPOWERED ili kuhakikisha kuwa
TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA KATIKA MAMBO YOTE (Warumi 8:34-38).
Ni maombi yangu kwako, ifikie mahali ambako haijalishi ni
hali gani inakujia au unapitia, ila kutokana na wingi wa NEEMA YA KUKUSAIDIA
WAKATI WA MAHITAJI usiweze kusikia joto na maumivu ya hilo jambo.
Lolote litakalotokea maishani mwako, likukute tayari una
NEEEMA YA KUKUSAIDIA DHIDI YA HILO HITAJI.
Kabla hitaji la divai kuisha kule Kana, tayari Yesu alishakuwa
na NEEMA YA KUMSAIDIA kutatua hilo tatizo.
Walipouliza cha kufanya hakujiuliza, neema ilikuwepo tayari
kukomesha hilo hitaji.
(Yohana 2:1-11).
Wakati alipohitajika kulisha wanaume elfu tano na wanawake
na watoto, bila kujali hali ya kidogo kilichokuwepo, kwa sababu NEEMA YA
KUMSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI ILIKUWEPO, alichukua wale samaki wawili na mikate
mitano na kutoa suluhu.
(Mathayo 14:15-21).
Nakuona ukitembea katika neema hii ya ajabu.
NEEMA YA KUKUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI.
Mwl D.C.K
No comments:
Post a Comment