Monday, 15 February 2016

THE POWER OF COVENANT, AGREEMENT AND RESPONSIBILITY IN FAITH.

 Nimekumbushwa na Roho Mtakatifu kutoa somo hili
  1.  Nini maana ya covenant
  2.  Agano
  3.  Maana yake ni nini
  4.  What is agreement?
  5.  And what is responsibility
 Akina nani wanaingia katika agano, makubaliano na kupeana majukumu?
Wanaongia katka makubaliano wanakuwa na sifa gani
 Nimefundisha somo hili katika fellowship mbalimbali na wengi wamesonga mbele kiroho
kwa kawaida  Wanaopatana
, wanaongia katika agano au makubaliano ni kwamba wanakuwa na common understanding
Wanafanya hivyo in order to achieve the Planned goals
 Inapotokea mwingine kati ya hao wanaokubaliana anaenda kinyume maana yake
  1.  Anavunja agano
  2. Ana asi
 Alleluiaaa Nini maana ya kuasi?
Mungu ananiambia kuasi ni sawa na kuwa mchawi, ukaidi ni sawa na ukafiri
 Ukafiri ni upingaji
 1samwel 15:23
Labda nikutembeze katka maandiko kidogo ili uelewe hili
Yoshua 7 :1
 1 Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli.

 Ni kipindi ambacho Yoshua anawaongoza waisrael kuingia kanaani , Kuna falme kubwa na zenye nguvu walizokutana ikiwemo yeriko na Ai
 Ili kushinda uvamizi huo yoshua anaweka agano na waisrael
18 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.
Yoshua 6 :18
 Sasa kuna MTU mmoja jina lake akani kabila LA Yuda . baada ya kuvamia akachukua hivyo vitu akfu akavificha
Neno la Mungu linasema hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana waisrael
Hebu elewa hapa hasira ya Bwana haijawaka juu ya akani Bali juu ya Israel yote
 Nini kikatokea ?
 5 Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Joshua 7:5
 Walipoingia vitani waisrael wanapigwa
 Yoshua akaingia katka maombi kumlilia Bwana na Mungu anajibu hivi
 11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.
Yoshua 7 :11
 Nani huyo aliiba?
 21 Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Yoshua 7 :21
Ni maneno ya akani baada ya kuulizwa na yoshua
Je Mungu akafanya nini?
 12 Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Yoshua 7 :12
 Majibu ya Mungu kwa Yoshua
 Ukiendelea kusoma sura nzima ya 7
 Akani anakamatwa na kupigwa mawe pamoja na familia yake yote na mifugo yake yote na kuchomwa moto
 Sasa naimani umeanza kuelewa
Unapokubaliana kwenye chochote kinachomhusu Mungu. Unaposhidwa kutekeleza uwe unauhakika unaliangusha kanisa au fellowship nzima
 Kuna watu ambao kwa sababu siyo kiongozi au hafahamiki basi anatenda anachotaka
Mfano tumekubaliana uzinzi, uchoyo, usengenyaji. Chuki haviitajiki ndani ya kanisa Wewe bado unafanya
 Nakwambia sasa acha hicho unachokifanya ambacho ni kinyume na makubaliano
  1.  Unaliangusha kanisa
  2.  Unaiangusha fellowship
  3.  Katka Jina la Yesu Kristo acha hiyo tabia ya kutokutoa zaka. Sadaka. Sehemu ya kumi. Ni wizi huo . unamwibia Mungu
 Asante ewe Roho mtakatifu katka somo hili
Nikutakie ewe msomaji utume mwema katika JINA la YESU kristo.

No comments:

Post a Comment