kufunga nini?
kuomba ni kitu gani?
kuomba na kufunga kuna uhusiano gani?
katika hili zipo sababu nyingi sana kwa nini tunafunga na kuomba. kwa leo ngoja nikupitishe katika maandiko , uweze kuelewa hili na litakusaidia sana .BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO UTUTAZAME SISI WAJA WAKO , UELEWA WA SOMO HILI SAWASAWA NA MAPENZI YAKO. AMINA.
: 18 Yesu akamkemea
pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Mathayo 17 :18
19 Kisha wale
wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
Mathayo 17 :19
: 20 Yesu
akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia,
Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa
uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Mathayo 17 :20
: 21 [Lakini
namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Mathayo 17 :21
: Kuna magumu
mengi yanatukabiri yakiwemo kwenye huduma zetu na fellowship yetu kama hatutafunga na kuomba kamwe hatutafanikiwa
: Wengi wetu tumekuwa wazito kwenye kufunga. Ngoja nikwambie hata
wale wanaomtumikia rusifa ibilisi hufunga ili kupewa nguvu na kuonana na mkuu wao Huyo. Wewe
mwana wa Mungu kwanini unashindwa kufunga ? Je utashinda hiyo vita! Je mapepo yatakutii ? Jamani tubadilike
: Kuna mtu mmoja ambaye
alikuwa anamtumikia ibilisi
alishuhudia baada ya kuokoka na kusema alifunga siku 40 ili akaonane na
rusifa. Ili apewe nguvu na cheo. Ilipofika siku ya 36 alikatisha katka mkutano mmoja wa injili huko Kenya akashikwa na mchungaji
ndipo ikawa siku ya wokovu wake
: Je Wewe. Mwana Mungu?
: Tubadilike
: Ee Bwana Yesu
tujalie Imani
Amina.
ReplyDeleteAmina kaka edson
ReplyDelete