Tuesday, 15 March 2016

MAARIFA YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

                                      
                Imeandaliwa na luhwago shadrack c contacts 0764444277/0712105099
                                luhwagoshadrack17@gmail.com.

PDF HERE

Ndoto ni mtiririko wa picha zitembeazo katika akili ya mtu,pindi mtu huyo anapokuwa amelala. Ndoto huja pale mtu anapokuwa amelala,na ndio maana huwezi kumkuta mtu ambaye ajalala,mtu atembeaye kisha akuambie ya kwamba alikuwa anaota ndoto wakati anatembea.
Actually ndoto husubiri kupumzika kwa akili. Wakati mwingine
ndoto hutokana na shughuli na mawazo ya mchana “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;..."Mhubiri 5:3 “Wengi huota kwa sababu ya miangaiko ya mchana kutwa,wakilala tu pale akili inapopumzika,nao huota. Ndoto za namna hii huwa hazina maana.SIKU YA LEO NATAKA NIZUNGUMZIE NDOTO ZENYE MAANA…….amina.
Praise the lord, praise the lord, alleluia alleluia.
Wapendwa katika kristo kuna kitu kinaitwa NDOTO na kingine kinaitwa MAONO.
Ni kwamba NDOTO kila mmoja anaota lakini siyo MAONO, Since kwenye maono you must have ROHO MTAKATIFU WA MUNGU.
Sasa leo nazungumzia NDOTO kitu ambacho kinaendelea kuwa shida kweli katika maisha yetu wakati wa usingizi. Na ijulikane kuwa MUNGU anaongea na binadamu kupitia ndoto lakini kuna ndoto pia za kiibilisi.MUNGU ANAPOONGEA NA BINADAMU KUPITIA NDOTO NI KWAMBA ANATAKA HUYO BINADAMU AJUE KILE KINACHOENDELEA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO either kibaya kwake au kinzuri.
KIBIBLIA Ndoto zilizotoka kwa Mungu zilikuwa wazi na zenye kupatana na akili, na zilikuwa na ujumbe kuhusu jambo Fulani.
Katika Hesabu 12:6 imeandikwa ‘Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, NITASEMA NAYE KATIKA NDOTO’. Ndiyo, Mungu husema kupitia ndoto, kwa kuwa ndoto ni lugha s.luhgo
ya picha tena rahisi ya mawasiliano kwa yeye kufikisha ujumbe wake na hivyo kumsaidia mtu aelewe mpango wake (Mungu) kwenye maisha yake na hivyo kufanya maamuzi muafaka.
Pia katika Ayubu 33:14 imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani’. Hapa Biblia inatueleza kwamba kumbe ndani ya ndoto kuna sauti na hivyo mtu anaweza kuisikia sauti ya Mungu kupitia ndoto, ingawa si ndoto zote huambatana na sauti. Ndoto huja pale mtu anapokuwa amelala usingizi na hili lina maana, mtu anahitaji muda na mazingira bora ya kulala ili Mungu aweze kusema naye kwa njia hii. Ndoto inaweza kuja kwa mfano wa hadithi au tukio lenye kisa au uzoefu fulani ndani yake.
Endapo, katika ndoto ambayo ni ya kutoka kwa Mungu, ukiona unaongea, maana yake Mungu anakuonyesha nini cha kusema, kufanya au kuomba punde utakapoamka. Kuomba baada ya kuamka au kushtuka ni LAZIMA ili kuhakikisha zile za kutoka kwa Mungu zinatimia na zile za kutoka kwa Shetani zinazuiliwa.Jambo la msingi ni lazima mtu ajifunze kutafsiri ndoto anayoiota kama sauti ya Mungu kwa kuwa ndani ya ndoto kuna ujumbe. Kuwa na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ndio msingi muhimu wa kuelewa na kufasiri ndoto unazoota. Rejea mifano ifuatayo ndani ya Biblia ili kuelewa zaidi njia hii.
Mungu anasema na Abramu kuhusu uzao wake (Mwanzo 15:12), Mungu anasema na Sulemani juu ya mambo mbalimbali (1Wafalme 3:5-13), Mungu anamonya Abimeleki kuhusu mke wa Abramu (Mwanzo 20:1-7), Mungu anamuonya Yusufu, asimwache Mariam (Matahyo 1:20), Mungu anasema na Yusufu kuhusu ulinzi wa Yesu dhidi ya hila za Herode (Mathayo 2:13).
FUNDISHO KWA SISI WAOMBAJI
Ukitoka tu kwenye maombi au maombezi au huduma ya derivalence jaribu kupata sehemu tulivu kabisa ili ulale kwa dakika kadhaa ili Mungu aweze kuongea na wewe katika NDOTO ukitoka kwenye maombi hasa ukijisikia usingizi inabidi ulale usijinyime.
Wengi wetu tumekuwa tukitoka kwenye maombi tu tunakurupuka tunaendelea na shughuli zetu saa hiyohiyo. Namshukuru Mungu sana katika hili nilikuwa sijui ila sasa ivi Mungu ananitumia sana katika NDOTO.
Kwa uelewa wangu mdogo wa maandiko matakatifu sijaona mahali ambapo shetani anaongea na binadamu,,,, sasa kwa nini ndoto za kiibilisi?....wakati mwingine Mungu anajaribu kumtaarifu mwana wake (binadamu) juu ya mpango na mambo anayofanya ibilisi juu yake, lakini shetani pia anatabia ya kuchukua binadamu usiku na kuondoka nao spiritually..
Sasa kwa sababu Roho ya binadamu huyo aliyechukuliwa ipo bado hai , inaendelea kuona kile kinachoendelea but unconciuosly. Ndoto za namna hii ni vigumu sana kukumbuka asubuhi au ukiamka, au baada ya kushituka nafsi yako inafadhaika sana. Na kinachofanyika ni kwamba wachawi au shetani na wakala zake wakimhitaji binadamu wanaita jina tu na huyo popote alipo hata kama amelala anatokezea hapo walipo na atashiriki kila wanachomuamuru afanye na kisha watamuachia arudi kwake, sasa wakati huo kwa binadamu huyu aliyechukuliwa kwake anaendelea kuota ndoto na itabaki kuwa ndoto kumbe ni live.
INAWEZEKANA ULISHAWAHI KUOTA NDOTO KAMA:
Unashiriki mazishi ya watu wengi usiowajua, upo angani sana na unataka kudondoka, unakula nyama na watu wengi usiowajua, unanyoshesha mtoto wakati wewe huna mtoto na huna uwezo wa kuzaa, unakimbizwa na kundi la watu usiowajua, upo makaburini, unakutana na watu waliokufa, unaota unalima na ukiamka kweli unakuta umechoka, unafanya mapenzi na mtu usiyemjua, unaota unakimbizwa na mnyama wa ajabu na unajitahidi kukimbia lakini hufiki mbali as if miguu yako imefungwa, unatapika vitu vya kutisha sana na nyingine nyingi zinazofanana na hizo………..
Katika hali ya ndoto za namna hii kila ndoto ina maana yake lakini kwa ufupi ni kwamba mtu anayeota ndoto za namna hii NGUVU ZA SHETANI BADO ZINAMFUATILIA yaani ibilisi bado anamchezea, either ibilisi bado anamililki jina lake, nyota yake, afya yake, maisha yake kwa ujumla. KUMBUKA wanapokuhitaji wanakuita JINA LAKO. Sasa chakufanya wewe mwenye kuota ndoto za namna hii KUOKOKA NI LAZIMA. NA KISHA FANYA MAOMBI YA NGUVU YA KUFUTA JINA LAKO KWENYE ILE ORODHA ALIYONAYO IBILISI yaani jina lako wasilione kamwe na hata wakikuita wasikuone. Jambo la pili ni kwamba kila unapoenda kulala omba kwa Mungu njozi zinazotoka kwake tu,
nenda kinyume kabisa na ndoto za kiibilisi. Na wakati mwingine kwa uliyeokoka na kuendelea kuota ndoto za namna hii KUMBUKA KUANZA NA TOBA NA REHEMA KWANZA pengine hujawa sawa kiroho.

GET PDF HERE

1 comment: