BY LUHWAGO SHADRACK C PDF HERE>>>
What is a territory?.
What is in the territory?
Why to fight for your territory?
Hii ndiyo maana ya kawaida kabisa ya neno Territory is (an area of) land or sometimes sea, which is considered as belonging to or connected with a particular country or person.
KATIKA HII DIFINITION KUNA MANENO KAMA connected, na belonging.ni maneno ambayo yamenisukuma siku ya leo kutoa somo hili kwako mpendwa Taifa Teule la Mungu.
Kwa hali ya kawaida kila mmoja wetu ana miliki
na vitu mbali mbali ambavyo either ni direct connected au indirect connected to him or her.
Kwa wewe uliyeokoka , kwa wewe uliyechagua fungu lililojema , kwa wewe uliyempokea na kumkiri Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ni saa yako sasa kusikiliza kwa makini somo hili.
Kwa uliyemkiri Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako hakika miliki na himaya yako ni WATOTO WAKO, WAZAZI WAKO, ELIMU YAKO, AFYA YAKO, MASHAMBA YAKO, MARAFIKI ZAKO, JUMUIYA YAKO, NDUGU ZAKO(MJOMBA WAKO, SHANGAZI YAKO, BIBI NA BABU YAKO, MDOGO WAKO, MAMDOGO WAKO, NDOA YAKO, UKOO WAKO), mafanikio yako kiuchumi na Nyanja zote kijamii na kisiasa na mengine yanayofanana ya hayo.
KWA TAARIFA TU NI KWAMBA USIPOJUA KUWA HIZO TAJWA HAPO JUU NA NYINGINE ZINAZO FANANA NA HIZO NI MILIKI NA HIMAYA YAKO UWE UNA UHAKIKA KABISA SHETANI ANATAWALA
Katika utafiti wangu nilioufanya kwa kipindi cha hivi karibuni ni kwamba watu wengi sana wamefanikiwa kiroho lakini familia zao na koo zao, ndugu zao, wazazi wao, mashamba na mifugo yao n.k bado inashida.kuna magonjwa mbalimbali yanayoshambulia familia zao na ndugu zao, koo zao zimejaa mauti(vifoo visivyo na kikomo) LAKINI YEYE AMEOKOKA.
Je ! tatizo liko wapi ?
Aliyeokoka amesahau kushughulikia kisawasawa himaya na miliki zake.
LABDA NGOJA NIKUPITISHE KATIKA MAANDIKO…….
MARKO 5:6-10
6Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia akapiga magoti mbele Yake. 7Akapiga kelele kwa nguvu akisema, ”Una nini nami, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu? Ninakuapisha kwa Mungu, usinitese! ” 8Kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia,‘‘Mtoke mtu huyu wewe pepo mchafu!”
9Yesu akamwuliza, ‘‘Jina lako ni nani?’’
Akamjibu, ‘‘Jina langu ni Legionia, kwa kuwa tuko wengi. ” 10AKAMWOMBA SANA YESU ASIWAPELEKE NJE YA NCHI ILE.
Version nyingine ya BIBLIA imeandikwa 10. AKAMSIHI sana Yesu asiwapeleke nje ya nchi ile.
NENO KUSIHI NI ZAIDI YA KUOMBA. Huyu pepo anakubali kutoka kwa huyu mgelasi lakini anataka aendelee kubaki kwenye nchi ile, yaani huyu pepo anachotaka aendelee kuishi kwenye mazingira ya hapohapo(ugerasini).
Sasa unapookoka unawekwa huru katika maisha yako, ila anachokifanya shetani ni kuhamia kwenye miliki zako. Watu wengi baada ya kuwekwa huru na Yesu Kristo, kwa kweli ibilisi amekataa kutoka kwenye himaya tajwa hapo juu.
Kitu kingine ni kwamba ibilisi ana shughulika na hatima yako na siyo kingine hebu tazama
MARKO 4:35b-37
NA TUVUKE MPAKA NG'AMBO. 36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji
Siunaona hapo YESU aliposema tu NA TUVUKE MPAKA NG'AMBO maandiko yanatuambia ikatokea DHORUBA. ibilisi alijua kabisa kwamba Yesu akivuka ng’ambo atamuweka huru mgerasi ndiyo maana that’s why alileta dhoruba wasifike na baada tu ya kuvuka ng’ambo Yule pepo akasema UNA NINI NAMI, YESU MWANA WA MUNGU ALIYE JUU?.
Hadi hapo nafikiri umeanza kuelewa nini kiini cha somo hili, popote na wakati wowote unapoamua kuokoka yaani kuvuka ng’ambo uwe na uhakika kabisa kuwa KUZIMU NZIMA INAINUKA mfano dhoruba tunayoiona hapa.
Na kama nguvu hizi za kuzimu zitashindwa kukuangusha basi zinang’ang’ania himaya yako au miliki yako TAJWA HAPO JUU.
NB shetani haogopi elimu yako, biashara yako, au huduma yako ya kanisa unayofanya ila anaogopa EFFECT OF YOUR EDUCATION, BUSINESS NA effect ya huduma yako katika kanisa.
Mfano ukipata elimu au biashara nzuri au kazi nzuri actually utakuwa na pesa , SASA KUJA MOJA KWA MOJA KWAKO HAWEZI KWA MAANA UMEOKOKA ANACHOKIFANYA NI KUSHUGULIKA NA NDUGU ZAKO AU WAZAZI WAKO EITHER KWA KULETA MAGONJWA AU VIFO HALI AMBAYO ITAPELEKEA HELA NA PESA YAKO KUTUMIKA TUMIKA TU PASIPO SABABU.
HALI HII INAWEZA KUKULETEA HATA UCHUNGU MOYONI MWAKO KIASI AMBACHO IBILISI NAYE ANAWEZA KUKUPATA VINZURI AKUINGIE HATA WEWE ULIYEOKOKA AKUSHUGHULIKIE.
Ni wakati wakujiuliza mwenyewe sasa dhoruba ngapi zimeinuka juu yako tangu ulipoanza haya maisha ya wokovu,
Kwa maana shetani anajua ukiokoka utawaweka huru hata ndugu zako, thus anachokifanya ni kuinua dhoruba zitakazo kufanya usifanikiwe.
Last message to you:
1.USIPOOMBA KWA AJILI YA HIMAYA YAKO SHETANI ANAINGIA
2.SHETANI HANA SHIDA NA UNACHOKIFANYA ILA TU KILE UNACHOKIPATA (FRUITS)
3.MGERASI ALIISHI MAKABURINI LAKINI HAKUWA MAITI : check your surrounding yaani nani anakuzunguka
.SHETANI ANAJUA KABISA HUYU MTU ANAJUA AU HAJUI MILIKI YAKE
4.HATA KAMA SHETANI AMENG’ANG’ANIA MILIKI YAKO FANYA MGOMO(RIOTS) WA KIROHO WA KUMWONDOA. REMEMBER IT IS WRITTEN NEVER GIVE OPPORTUNITY TO THE DEVIL(USIMPE SHETANI NAFASI).
5. ILIPOFIKA DHORUBA WANAFUNZI WALIMWAMUSHA YESU NA AKAITULIZA ILE DHORUBA sasa katika dhoruba zote ulizo nazo katika safari yako ya kiroho nakusihi MWAMBIE YESU AAMUKE NA ATAKUSAIDIA.
MUNGU NA AWABARIKI SANA.
BY luhwagoshadrack17@gmail.com
0764444277/ 0712105099
😃😃
ReplyDeletemr, tete umefurahi au hujaelewa nielezee tena? picha hapo juu nashindwa kuelewa maana yake..au type maneno
ReplyDelete