Friday, 23 November 2018

MAISHA YA UMILELE



BY APOSTLE SHADRACK LUHWAGO
0764444277  or 0712105099

BWANA YESU APEWE UTUKUFU, TAIFA TEULE LA MUNGU
Ninayo furaha kubwa siku ya leo kukuletea ujumbe huu ambao utakuwa chemichemi ya kufahamu makao yako ya milele, na namna ikupasavyo kutenda angali u hai hapa duniani
Ndugu zangu katika KRISTO YESU neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na ushirika wa Roho mtakatifu uwe nasi sote, kwa maana sisi hapa duniani Tu wapitaji/ wasafiri. Na imetupasa kuishi na kuenenda kama
msafiri.
Kwa maana Msafiri hujua wapi anakwenda!!!!!   Msafiri huchagua usafiri gani atumie ili afike sawasawa na anavyotarajia kufika ikitegemea umbali wa wapi anakwenda!!!!!!  Msafiri hawezi kutumia punda au trekta kusafiri kutoka Tanzania kwenda marekani ,kwa sababu punda au trekta haviwezi kupita kwenye maji.
Ndivyo ilivyo kwa sisi wana wa Mungu tuliopo hapa duniani , kwa maana aina ya Maisha, matendo , maneno na kuketi kwetu ndiyo chombo cha kusafiria kufika kwenye makao ya umilele. Ifahamike kuwa wanadamu imetupasa kujua kuwa KUNA MAISHA MENGINE baada ya MAISHA HAYA .  na MAISHA HAYA yaani ya hapa duniani yamefungwa na MUDA  angali MAISHA YALE MENGINE yamefungwa na UMILELE. Umilele huo yaweza kuwa MOTONI AU MBINGUNI(YERUSALEMU).
Imeandikwa katika kitabu cha 1 petro 2:11 – 12 kuwa ‘’ English:
Beloved, I exhort YOU as aliens and temporary residents to keep abstaining from fleshly desires, which are the very ones that carry on a conflict against the soul.
Swahili:  
“Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho”
Neno KUSIHI ni Zaidi ya kuomba ,lenye maana ya kusisitiza, na maandiko haya yanasema KUISHI KAMA MPITAJI NA MSAFIRI. Ipo siku itakapofika ambapo watu wataomboleza ya kwamba umeondoka yaani umekufa ,akina mama na watoto  watalia machozi kwa uchungu wakikumbuka fadhila zako kwao lakini wewe kumbuka utaingia either MOTONI AU MBINGUNI kwa kadri ya matendo yako ya hapa duniani. Kwa version ya kiingereza imeandikwa “ AS ALIENS AND TEMPORALY RESIDENTS) . watu wengi tumejisahau ya kwamba sisi hapa duniani tunapita. Tumekuwa tukiishi kwa mazoea , tukiamka na kula kama watu tuliofika tayari , kana kwamba tutaishi hapa duniani milele.
Kumbuka kuwa “ mtu ni NAFSI na roho anayeishi ndani ya nyumba” na nyumba hiyo ni MWILI, ipo siku mtu atatoka ndani ya nyumba hiyo na kurudi kwake kwenye makao ya umilele , either MOTONI AU MBINGUNI.
Wapendwa katika Kristo Yesu, moto wa milele upo, na si nadharia kwamba ni maagizo, JEHANAMU ipo , na inasubiri siku ya hukumu watu wote waliotenda maovu waingizwe humo pamoja na yule ibilisi shetani.
Imetupasa kujitengezea Maisha ya utakatifu angali bado wazima hapa duniani, bila kutafutiwa au kuombewa na wenzetu, kwani yule mwizi pale msalabani alijiombea mwenyewe kwa Yesu, na pia mfalme  DAUD katika uhai wake alijiombea mwenyewe,
Imeandikwa  katika ZABURI 39: 1-12 English: 4"Jehovah, please make me to know my end. What is the extent of my days? Let me know how temporary (frail) (destitute) I am”.
Swahili: “Bwana, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu”.

MFALME DAUD ANAJIOMBEA MWENYEWE KWA MUNGU ajulishwe mwisho wake kabla hajafa ili ajue alivyo mdhaifu na namna impasavyo kutenda. Hivyo mimi na wewe tuandae Maisha yetu kabla hatujafa kwani hakuna nafasi hata ya sekunde moja ya kuomba toba au rehema ukisha kufa. Hata wakikusindikiza kwa maombi ya ki-BISHOP au kwa sala maalumu , ninakwambia leo hayatakusaidia. Nafasi unayo leo ya kutafuta wokovu wa kweli utakaokufanya uwe na kibali siku ya mwisho kwa ajili ya makao ya milele.

Imeandikwa katika kitabu cha DANIEL 12:1-3 1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. 2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. 3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.

Kwa maana wanadamu waondokao katika dunia hii HAWAFI bali WANA LALA ndivyo itakavyokuwa siku ya mwisho kwa ajili ya Maisha ya UMILELE, miili ya watakatifu iliyolala chini ya ardhi itafufuliwa kwa shangwe na furaha na kuingia mbinguni, wakati miili ya wale waovu itaingia motoni kuunguzwa milele pamoja na shetani.

Imeandikwa katika kitabu cha UFUNUO WA YOHANA 20: 11- 15,  11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Ninahuzuni kubwa kutamka kuwa watu wengi hawataingia mbinguni, kwa maana maovu yameongezeka, uzizi , uchawi, ugovi, usengenyaji, kuabudu miungu mingine , ibada za sanamu , watu wamekuwa ni wapenda pesa na mali kuliko MUNGU, chuki zimeongezeka kila mahali, nasema pole kwa wewe unayetenda haya , kwa maana huwezi kumuona MUNGU siku hiyo na wala hutaingia mbinguni,

Maombi yangu ya leo kwako mwanadamu ambaye bado una nafasi ya kumjua na kumtafuta MUNGU aliye hai katika KRISTO YESU, ni  kwamba  geuka na umtumikie MUNGU kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote, na ndipo litapotimia neno lililoandikwa katika kitabu cha MATENDO YA MITUME 13: 36 ya kwamba English: "After David served his own generation by doing the will of God, DID FELL ASLEEP with his fathers. His body decayed”. Swahili: “Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu”.

MUNGU AKUBARIKI NA KUKUJAZIA NEEMA KWA SAFARI YAKO YA HAPA DUNIANI, KATIKA KRISTO YESU MWANA WA MUNGU ALIYE HAI
AMEN.

No comments:

Post a Comment