Wednesday, 18 January 2017

KIFO SIYO TUKIO BALI NI ROHO



                         SOMO: KIFO SIYO TUKIO BALI NI ROHO
Na apostle of JESUS CHRIST shadrack luhwago ,  luhwagoshadrack17@gmail.com  0764444277/0712105099, www.lshadrackc.blogspot.com
                          @naihubiri injili kwa kasi ya 4G@
BWANA YESU APEWE SIFA TAIFA TEULE LA MUNGU………………………
NINAWASALIMU WOTE KATIKA JINA LA YESU KRISTO..
ROHO YA MUNGU YU PAMOJA NAMI KATIKA KUKULETEA SOMO HILI LA
LEO YA KWAMBA  KIFO SIYO TUKIO BALI NI ROHO.
Kwanza Tuombe : BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO asante kwa kutupa muda na wakati huu ili tuweze kuelewa sisi waja wako yale uliyokusudia kutupa siku ya leo, ninakushukuru ewe muumba wa mbingu na nchi kwa uhai, mafanikio, na afya njema unayoendelea kutujalia, tunalitukuza jina lako kristo kwa rehema na neema unayoimimina kwenye maisha yetu,nasi twashuhudia ushindi katika vita, uponyaji na wokovu kwa jina lako kristo. ewe emanuel MUNGU pamoja na wanadamu, emanuel pamoja na huyu kijana na mzee, emanuel pamoja na kusanyiko hili, emanuel pamoja na wagonjwa wote ninakusihi uturehemu maana tumekutenda dhambi, nasi twaitazamia damu ya kristo itupayo ukamilifu katika yote. aachilia ROHO WAKO MTAKATIFU akafundishe haya uliyokusudia kwa waja wako huku ukimtumia mtumishi wako kama chombo, kwa mamlaka niliyopewa na kristo ninamfunga yule adui shetani katika anga, ardhi na maji  kote namimina damu ya kristo na kukabidhi himaya nzima ilindwe  na malaika MIKAEL, GABRIEL NA RAFAEL. ni katika  jina la YESU KRISTO tunaomba kwa kushukuru na kuamini , na kila mwenye pumzi aseme ameeen.
WAPENDWA KATIKA KRISTO NAWASALIMU TENA KATIKA PENDO LA MUNGU WETU WA MBINGUNI
SIKU YA LEO NIMETUMWA NA MUNGU KUONGEA NANYI NA KUWALETEENI UJUMBE KWAMBA KIFO SIYO TUKIO BALI NI ROHO, nimatumaini yangu kwamba uelewe kwa kiwango ambacho MUNGU amekusudia upate katika nyakati za maisha ya kizazi cha sasa .

Nini maana ya kifo?
Ni mwisho wa maisha ya kimwili au kiroho?
Kukosa au kutokuwa na uhai.?
Kutokwa na Roho / Pumzi?
Ø  Ni hali ya kufarakana au kutengana kwa vitu au hali zinazofanya uhai kuwepo. Kwakuwa Upo uhai wa aina tatu wa mwilini, nafsini na rohoni; vivyo hivyo na aina za kifo. Kifo au mauti ni Roho kamili na siyo tukio.
Ø  Sisi sote kwa wakati fulani, labda baada ya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu, tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu, yaani, kuwa na hisia ile ya upweke inayopita ndani yetu tunapoangalia kwa haraka kuona mwisho wa uhai wa mtu.
Ø  "Mavumbi ya Ardhi" + "Pumzi ya Uhai" = " Roho Hai"
Ø  Mwili Usio na Uhai + Pumzi toka kwa Mungu = Nafsi Hai.
Ø  Kila mmoja wetu anao mwili na akili inayofikiri. Kwa kadiri sisi tunavyoendelea kuvuta pumzi, tutaendelea kuwa nafsi hai, yaani, roho hai.
Ø  Mtu anapokufa kinyume cha hatua zile za uumbaji zilizoelezwa katika Mwanzo 2:7 hutokea "Nayo MAVUMBI huirudia ardhi yalikotoka, nayo ROHO [PUMZI YA UHAI] humrudia Mungu aliyeitoa." - (Mhubiri 12:7).
Kwa sababu kila chenye kimwili kina cha kiroho chake. Kimsingi  uumbaji ulianzia kwenye ulimwengu wa Roho yaani visivyoonekana viliumba vinavyoonekana vivyo hivyo kifo kinaanzia ulimwengu wa Roho kuja kwenye ulimwengu wa mwili.
Hebu tutazame kifo kilichotokea baada ya anguko kwenye hiki kitabu cha mwanzo 2:17
17lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.’ Hapa tunakutana na neno linalosema SIKU UTAKAPOKULA , kibinadamu baada ya kula tu tunda ilibidi hata adamu aanze kuchimba kaburi amzike eva , sasa alipoona kweli hajafa baada ya kula tunda akahisi Yule nyoka alikuwa sahihi aliposema “mwanzo 3:4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.” . hakika eva hakujua kuwa kifo ni Roho na bali ni  tukio, ndiyo maana baada ya kula akaona hajafa akapata ujasiri wa kumpelekea na adam asijue kilichokufa ni ROHO na siyo tukio.
Kama kifo ni tukio basi tusemeje , je MUNGU alikuwa muongo?  Kwamba watakufa?  Majibu yake utaona kuwa kifo siyo tukio bali ni Roho kamili na ndiyo tunayoita ROHO YA MAUTI IKAIINGIA DUNIANI baada ya anguko.
2wafalme 2: 21
Kisha akatoka akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, “Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ ”  mauti ndo kifo na ndiyo ROHO na siyo tukio na tazama hapa kwamba ROHO YA MAUTI ipo kwenye maji.
2wafalme 4:40-41
Mchuzi ukagawiwa watu, lakini walipoanza kula, wakalia, “Ee mtu wa Mungu, kuna mauti ndani ya chungu.” Nao hawakuweza kula.  41Elisha akasema, “Leteni unga,” akauweka ndani ya chungu na kusema, “Wagawie watu ili wale.” Wala hapakuwa na kitu cho chote chenye madhara ndani ya chungu” tazama hapa kuwa ROHO YA MAUTI IPO SUFURIANI.
Luka 1:79.
………. ili kuwaangazia wale waishio gizani  na katika uvuli wa mauti,  kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”………..
Luka 8: 54
……..Yesu akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” 55 Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara. Tazama hapa ROHO yake ikamrudia maana yake uzima wa huyu mtu ni ROHO YAKE.
Marko 14: 4
……Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa………kumbe moyo yaani ROHO inaweza ikafa huku mwili wa nyama ungali bado mzima.
Mathew 8: 22
Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, nawe waache wafu wazike wafu wao.’’ Je kama kifo ni tukio hawa watazikanaje?

BWANA YESU ASIFIWE ………
GROLY TO GOD , GROLY  TO GOD…..
Nimatumaini yangu umeanza kupata kitu pamoja na kuelewa kile ninachozungumza nawe saa hii.
Ngoja nikupe niliyowahi kukutana nayo kwenye huduma ya kufunguliwa…  siku moja ambayo nilikuwa nafanya huduma ya kufunguliwa(derivalence), ya mtu aliyekuwa na mapepo na majini na mizimu na nguvu za kichawi , maombi ya kuvunja yalipoanza mapepo yalilipuka na kusema huyu tumeshamuua na matanga tumeshafanya kama wiki mbili hivi zilizopita, na kaburi lake tunalo kwani tulichimba sisi wenyewe…….
Mengine yakasema unajisumbua tu kumwombea kwani hawezi kupona tumeshamuua…..  
Nilipomaliza huduma anashangaa kwanza kuwepo yeye kwenye eneo hilo la maombi, lakini pia aka nambia eti hakumbuki chochote alichokifanya ndani ya siku kadhaa hususani tangu augue (yaani toka siku ile kwenye ulimwengu wa roho walipomzika basi vivyo hivyo kimwili akasahau kila kitu), nikamuuliza kama hakumbuki chochote sasa alikuwa wapi ? akanijibu kwamba alikuwa safarini na wenzake wengi tu ambao hawafahamu. kumbe unaposhuhudia kuwa leo Fulani amefariki na tunamzika kaburini actually KIROHO inakuwa ilishatokea zamani sana. Hii haijalishi kwamba hicho kifo ni cha KIMUNGU AU KISHETANI….Na ndiyo maana watu wengine huota kifo chake kabla ya kufa.
Hususani pale ambapo binadamu anatenda tu dhambi basi kwenye ulimwengu wa ROHO mtu huyo anaoonekana ni mfu.( it looks a dead body) EFESO 2: 1--Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, …………
Niliwahi kukutana na mtu mmoja ambaye ameokoka na kuanza kusimulia yale aliyokuwa akifanya kipindi hajaokoka kwani alikuwa mchawi, jambo mmojawapo alieleza namna ambavyo wanamuua mtu katika ulimwengu wa roho na pia namna ya kujua kuwa mtu huyu au Yule amekufa kifo cha KIMUNGU AU KISHETANI.    
Ukielewa somo hili hakika hutashangaa unaposikia wafu wanafufuka au wewe mwenyewe kama mtumishi wa MUNGU unaouweza wa kufufua wafu.
Watumishi wengi sana tumefanikiwa kuondoa magonjwa kwa uwezo wa JINA LA YESU KRISTO lakini kwenye kipengele cha kufufua bado tupo nyuma,, kwa sababu nisomapo biblia naona kuwa popote pale ambapo mtu alikaribia kufa au kufa basi wahusika walitafuta huku na huku ili kupata watumishi wa MUNGU  ili arejeshe uhai kwa aliyekufa, na hii ilifanyika kabla ya kwenda kuzika….. lakini hii imekuwa tofauti kwa kizazi cha leo kwani mtu akifa tu basi tunaridhia na kuishia kuomboleza huku tukisema  BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,  MUNGU AMPUMZISHE  MAHALI PEMA PEPONI,  MUNGU AMPE RAHA YA MILELE  na maneno kama REST IN PEACE, na mengine yanayofanana na hayo . kiukweli hii imepelekea hata shetani akaiona fursa ya kuleta vifo akijua tu kwamba hawa waliobaki watachukulia POA.
Kwa kumalizia niseme hivi : wako wengi sana binadamu ambao ni DEAD BODY, yaani huyu katika ulimwengu wa ROHO   akina watakatifu wa MUNGU, malaika na jeshi la mbinguni pamoja na yeye mwenyewe   MZEE WA SIKU yaani MUNGU MWENYE ENZI wanamuona ni dead body is eating, moving, walking, praying, talking, preaching gospel, studying. Now ask yourself  AM I A DEAD OR LIVING BODY?
Wako wengi pia ambao wamekufa roho zao lakini wanatembea barabarani, wanafanya kazi maofisini, mfano wazinzi, walevi, wasengenyaji, wachoyo, wachawi, wavaaji mavazi mabaya hawa wote ni DEAD BODY katika ulimwengu wa ROHO.
Wako ambao pia wameumizwa roho zao kiasi cha kufa yaani mioyo yao imejaa uchungu(hasira iliyochacha) natamka rasmi kwamba KRISTO YUKO HAPA KWA AJILI YAKO . maandiko haya yametimia kwenye mioyo yenu siku ya leo ya kwamba…Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ 8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. (Mathew 10:7)
OKOKA KUBALI NA KUMPOKEA YESU KUANZIA LEO, MKABIDHI MAISH YAKO NA VYOTE VILIVYOKUFA MAISHANI MWAKO VIKIWEMO NDOA YAKO, KIZAZI CHAKO, FAMILIA YAKO, KAZI YA MIKONO YAKO, WAZAZI NA NDUGU ZAKO, ELIMU NA AFYA YAKO NA MOYO WAKO HAKIKA YESU KRISTO ATAVIFUFUA NA UTAONEKANA HAI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NA SIYO DEAD BODY TENA. Kwa maelezo zaidi nitafute kwa mawasiliano hapo juu na  MUNGU kupitia mtumishi wake atakuhuisha.
           Asante ROHO MTAKATIFU KWA UAMINIFU WAKO
                 Mungu awabariki katika JINA LA YESU KRSITO.

No comments:

Post a Comment